HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 27 julai 2010
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Wagosi kumpeleka Sugu bungeni


na Ruhazi Ruhazi

 

KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga, limetoka na kitu kipya kiitwacho ‘Sugu Nenda Bungeni’, ukiwa ni wimbo maalumu kwa ajili ya kumpigia debe msanii huyo aliyechukua fomu ya kuwania ubunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini jana, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, alisema wameamua kuacha kazi zao ili kumfanyia kampeni Sugu kutokana na kuukubali uwezo wake.

Walisema kuwa wanamfahamu vilivyo Sugu alivyopigania haki na mtetezi wa wanyonge, hivyo wanaamini akifika bungeni atakuwa na nafasi kubwa ya kuwatetea wananchi wa Mbeya.

“Tumeachia wimbo mpya wa ‘Sugu Nenda Bungeni’, tumeamua kumkampenia Sugu ili aingie bungeni tukiamini atawawakilisha vema wananchi wa jimbo hilo,” alisema Mkoloni.

Alisema wanatarajia wimbo huo utawasaidia wananchi wa jimbo hilo kumfahamu vema Sugu na kumpitisha katika chama chake na baadaye wamchague kuwa mbunge wao, atakayewaletea maendeleo ya kweli.



juu