HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 27 julai 2010
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Elimu ya uzazi wa mpango yawafikia wafugaji


na Halfani Lihundi, Babati

 

IMEBAINIKA kuwa jamii ya kifugaji wilayani Babati, Manyara imeanza kuwa na uelewa mkubwa juu ya dhana ya afya ya uzazi wa mpango baada ya juhudi za uelimishaji zilizofanywa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wilayani humo.

Hali hiyo imedhilika hivi karibuni wakati jopo la waandishi wa habari kutoka Kanda ya Kaskazini kutembelea baadhi ya vijiji wilayani humo kwenye ziara maalumu iliyoandaliwa na Shirika la Engender Health ya kuchunguza jinsi jamii hiyo ilivyopokea njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Wakizungumza na wanahabari, baadhi ya wakazi wa Kata ya Garapo wakiwemo wanawake ambao kwa kiasi kikubwa ndio waathirika kama uzazi wa mpango usipofuatwa, walisema kabla ya wataalamu kuwafikia wakazi wa vijiji vya kata hiyo hawakuwa wanaamini juu ya utendaji kazi wa njia hizo za kisasa za uzazi wa mpango.

Mmoja wa wanawake hao Naseriani Soinge, mama wa watoto watano, alisema kabla ya kupatiwa elimu ya uzazi wa mpango walikuwa wanatishwa kuwa njia hizo zinasababisha mwanamke kufariki dunia muda mfupi baada ya kutumia.

Naseriani alisema vitisho hivyo vilimtawala kiasi cha kuamini kuwa njia hizo si sahihi, lakini baada ya kuona baadhi ya wanawake kijijini kwao Songambele kuzitumia na kugundua kuwa hawakupata madhara hivi sasa yupo tayari kuanza kuzitumia.

Naye Nanyakwa Merineki, mkazi wa Kijij cha Singe, alisema kuwa amekuwa akitumia njia za asili za uzazi wa mpango kwa zaidi ya miaka mitano sasa lakini kwakuwa sasa amekwisha kupata elimu juu ya ubora wa njia za kisasa ameamua kuzungumza na mumewe ili watumie njia hizo.

Kwa upande wake, Ofisa Muuguzi Mkuu wa Zahanati ya Garapo, Alphonsina Matingo, alifafanua kuwa pamoja na wakazi hao kuzikubali njia hizo bado kuna changamoto nyingi zinazowakaili, ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo wa wazee wa kimila juu ya umuhimu wa njia hizo hasa njia ya kuwekewa kitanzi.



juu